Ukengee in Swahili

Newsflash

19 novemba 2010

by Gerda Kuiper

Tarehe ya 17 mwezi wa novemba, Ukengee Foundation ilikuwa na sherehe ya kufungua darasa la kompyuta kwenye Lindi Secondary School. Mgeni rasmil alikuwa RAS wa Lindi, aliyewakilishwa na msaidizi wake. Pia, watu watatu wa halmashauri la Ukengee ya Uhollanzi walikuja Tanzania kwa shughuli hiyo: Marijke Blom, Ronald Blom, na Hans Wilbrink. Zaidi kulikuwa na wageni wengi wa shule nyingine, wakilishi wengine wa serikali, Mr. Mng'umba na Shekhe Mushungana wa Solar Board yetu, na walimu na wanafunzi wengi wa Lindi Seco. Sherehe ilifurahisha sana. Tulisikiliza hotuba zenye busara sana; wanafunzi wa Lindi Seco waliimba na walicheza muziki; na washindi wa Ukengee Computer Competition, ambao waliandika essay kuhusu faida za kompyuta, walipata zawadi zao. Habari zaidi inapatikana (kwa Kiingereza) katika sehemu 'news' na picha za sherehe zitawekwa kwenye sehemu za 'Photos'.


About Ukengee
Ukengee Foundation ya Uhollanzi inalenga kuweka kompyuta na internet kwenye shule za sekondari mkoani Lindi nchini Tanzania. Internet ni muhimu sana kwa kupata taarifa, kwa kuboresha elimu, na kwa kuongeza nafasi za wanafunzi wa shule hizo.
Lakini katika mkoa huo, hali si nzuri kwa kompyuta kwa sababu ya joto na vumbi.
Kwa hiyo, Ukengee inasaidiwa na Inveneo. Shirika hilo linatengeneza kompyuta maalum kwa hali ngumu.
Zaidi, kompyuta hizo zinapata nishati ya jua. Kwa hiyo, shule bila umeme zinaweza kutumia kompyuta hizo pia.

Sasa hivi, Ukengee foundation ina miradi minne mkoani Lindi.
Shule ya kwanza iliyopata kompyuta mwaka 2009 ipo Kilwa Masoko. Mpunyule Secondary School Mandawa na Lindi Secondary School zilipata kompyuta baadaye. Shule ya wasichana kijijini Ilulu itapata kompyuta mwishoni mwa mwaka 2010. Wanafunzi wote wa shule hizo, na pia wanafunzi wa shule zinazozingira, watapata masomo ya kompyuta. Baada ya kumaliza miradi hiyo, wanafunzi elfu tano wataweza kutumia kompyuta. Ukengee foundation inalenga kwa kuweka kompyuta kwenye shule 35 zaidi miaka ijayo.

Ukengee foundation ina halmashauri Uhollanzi, lakini kazi nchini Tanzania inafanyikiwa na Ambassador Christopher Nyunza. Kutoka Oktoba 2010 mpaka Januari 2011, atasaidiwa na Gerda Kuiper. Gerda anatoka Uhollanzi, lakini alikaa Lindi mjini kwa kufanya utafiti. Amemaliza masomo yake, na anataka kurudi Lindi sasa kwa kuwasaidia wanafunzi pale.

Ukitaka kujua zaidi kuhusu Ukengee foundation, utumie barua pepe: info@ukengee.org